Ads

test

Friday, February 17, 2017

QUEEN LATIFAH KUTUNUKIWA TUZO HII KUBWA YA HESHIMA IJUMAA HII

Msanii, mwigizaji na TV na movie Producer kutoka Marekani Queen Latifah ni miongoni mwa mastaa watakaotunukiwa tuzo za heshima na “The American Black Film Festival Honors” weekend hii.
Msanii huyo ambaye anawania tuzo kubwa ya ‘The Oscars Awards’ mwaka huu anatarajia kupokea tuzo ya Entertainment Icon Award kwenye sherehe hizo za American Black Film Festival zitakazofanyika jijini Los Angeles, Marekani Ijumaa hii.
Queen Latifah
Kwa Mujibu wa pilotonline, Queen Latifah alifunguka juu ya tuzo hiyo, Queen Latifah alidai amefarijishwa sana na heshima hiyo aliyopewa na inampa nguvu ya kuendelea kufanya anachokifanya kwenye Entertainment industry.
Ukiachilia tuzo ya Oscar anayowania mwaka huu, Queen Latifah ameshawahi kuchaguliwa kuwania tuzo kubwa za filamu nchini Marekani, ‘The Emmy Awards’ na pia ameshawahi kushinda tuzo ya ‘The Golden Globe’.
Tuzo za The American Black Film Festival Honors zitaruka LIVE siku ya Ijumaa 22 Feb 2017 (tarehe 20 Feb. 2017 kwa nchi za Kiafrika) kupitia channel ya BET. Wasanii wengine wanaowania tuzo hizo ni pamoja na Terrence Howard maarufu kama Lucious Lyon kwenye series pendwa ya EMPIRE.

No comments:

Post a Comment