Tanzania imebarikiwa kuwa na vipaji lukuki, ukizungumzia mpira wa miguu wapo vijana wanaowakilisha vemaTaifa letu ughaibuni akiwemo Mbwana Sammata (Sama goal), Thomas Ulimwengu, Adam Nditi na wengine wengi. Halikadhalika kwenye muziki wapo vijana hodari wanaojua kutumia sauti zao vizuri kughani mashairi na kumfanya shabiki kutikisa kichwa kuashiria ameikubali kazi ya msanii husika.
Nimekuandalia orodha ya wanamuziki 10 wa kiume ambao wana sauti za mvuto, orodha hii imezingatia uwezo binafsi wa mwanamuziki katika kupangilia sauti kwenye mashairi na uwezo wa kuimba muda mrefu bila sauti kuathirika.
10. LINEX
Namba 10 inashikiliwa na kijana kutoka Kigoma Linex a.k.aSunday Mjeda. Sauti ya linex akiimba ni kama inakwaruza hivi lakini anaitendea haki sauti yake. Hachoshi ukimsikiliza huku ngoma zake nyingi zikiwa zimefanya vizuri ikiwemo Mama Halima, Salima, Moyo wa subira na nyingine nyingi . Ni muda sasa hatujasikia ujio mpya wa linex ila wahenga walisema kimya kingi kina mshindo, tusubiri mshindo wa Linex.
9. MO MUSIC.
Zao kutoka Mwanza , ni msanii mwenye uwezo mkubwa wa kuimba kama anavyojiita mwenyewe Mo Music (Zaidi ya muziki) hivyo analitendea haki jina lake . Wimbo uliomtambulisha vema kwenye ramani ya muziki unaitwa “Basi nenda” amabo ulimfanya apate show nyingi kiasi cha kutoroka masomo chuoni katika baadhi ya siku.
8. BARAKA THE PRINCE
Kutoka jiji la miamba Mwanza ndiko anakowakilisha, ni takribani miaka 2 tu tangu tumfahamu kama mwanamuziki wa kizazi kipya lakini uwezo wake wa kuimba ni mkubwa kiasi cha kuteka mashabiki wengi kwa muda mchache hasa kina dada kutokana na nyimbo zake zinazozungumzia mapenzi. Wimbo anaotamba nao kwa sasa ameshirikiana na Ali Kiba “Nisamehe”
7. BELLE 9
Kutoka mji kasoro bahari uso kwa uso na belle 9,uwezo wa belle ni mkubwa mno kama ataendelea kufanya vizuri basi atakumbukwa kama msanii bora zaidi wa kuimba kutoka Morogoro nyuma ya kina mzee Marijani na M’baraka Mwinshehe . Sumu ya penzi ndio ngoma iliyomtambulisha kwa mashabiki wa bongo fleva, kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya “Give it to Me”.
6. DIAMOND PLATUM
Huyu kijana ameleta mapinduzi makubwa kwenye kiwanda cha bongo fleva . Nani anabisha kuwa diamond kwa sasa ndio analiwakilisha vema taifa kwenye medani za kimataifa? Hivi karibuni alikuwa nchini Gabon kushiriki katika ufunguzi wa michuano ya Kombe la Mataifa Afrika. Juhudi na nidhamu ndio vimemfanya afike hapa alipo. Platnum anajua kubadilika kutokana na wakati kuhakikisha hachuji , kila siku anazidi kuwa mpya. Kwa sa ana record label yake WCB na amewasainisha wasanii kadhaa akiwemo Harmonize, Rayvanny na Qeen Darleen.
5. BEN POL
Bernard Paulo a.k.a Ben Pol mzaliwa wa Dodoma, kwa sasa unaweza kumuita mfalme wa rnb bongo. Ni mwanamuziki mwenye sauti ya mvuto , hachoshi kumsikiliza kutokana na jinsi anavyopangilia mashairi yake. Wewe unamkubali ben kwenye wimbo upi? Mimi namkubali zaidi kwenye wimbo aliomshirikisha Lina Sanga “ Yatakwisha”.
4. BARNABA BOY.
Barnabas Elias ndio jina alilopewa na wazazi wake ila kiwanda cha Bongo fleva kimemuajiri kwa jina la Barnaba boy. Umri wake bado unamruhusu kufanya makubwa zaidi, barnaba anaimba sana kiasi kwamba akiongea unaweza ukahisi kama sauti inakwaruza au ina mabadiliko, hiyo ni kawaida kwa wanamuziki wanaoimba sana kuwa na sauti Fulani hivi wakati wakiongea, msikilize Beyonce au Jarson Derulo wakiwa wanaongea utapata jibu. Barnaba kwa sasa anatamba na ngoma ya “Lover Boy” ila utamkubali zaidi ukisikiliza wimbo wa “I’m Sorry”.
3. BANANA ZORRO.
Kabla ya Christian Bela na Ali Kiba huyu ndiye alikuwa mkali wa masauti ila kwa sasa anashika nambari tatu, sifa nyingine huyu jamaa anaweza kuimba style zote iwe chakacha, rhumba, rnb, Pop, afro pop na aina zote zile, ni mtoto wa mwanamuziki mkongwe mzee Zahir Zorro.
2. ALI KIBA
Pamoja na kukaa kwenye game kwa muda mrefu, kiba ameweza kuhimili ushindani katika soko la muziki wa kizazi kipya, sauti yake haichuji, haichoshi kusikiliza na hakosei katika kuipangilia. Anaweza kuimba katika mahadhi ya Zouk na Afro pop. Ukitaka kumfaidi Kiba sikiliza wimbo wa “My Everything” . Mwaka 2016 ulikuwa wa mafanikio kwake kwani alijinyakulia tuzo mbalimbali ikiwemo tuzo ya BET aliyomshinda Wizkid kutoka Nigeria.
1. CHRISTIAN BELA
Kwa yeyote mpenda muziki wa ukweli hatasita kusema kuwa Bela ndiye mfalme wa masauti hapa Tanzania, jinsi atakavyoimba kwenye stage hutaona tofauti na audio uliyosikiliza kwenye radio, ana nyimbo ambazo ukisikiliza lazima umkubali. Moja ya wimbo unaokubalika zaidi ni ule alioimba na Ali Kiba “Nagharamia”.
NB: Bonus artist ni Peter Msechu.
Imeandaliwa na Dully Santo, Fb @dully santo & Insta dully_santo
No comments:
Post a Comment