Ads

test

Thursday, December 15, 2016

MMILIKI WA ZERO TO HERO RECORDS AWASHANGAA WANAOAMINI MIKOANI HAKUNA STUDIO BORA ZA MUZIKI

Mmiliki wa studio ya Zero to Hero Records iliyopo kahama ,mkoani Shinyanga , Newe Derefa ak.a super Newe, amewataka wasanii pamoja na wadau wa muziki nchini Tanzania kuondokana  na dhana ya kwamba mikoani hakuna studio nzuri na zenye ubora zaidi , kiasi cha watu kufunga safari kuelekea Dar  na kuacha studio kali zaidi mikoani.

Akiongea katika kipindi cha strengo Saturday cha Victoria fm, pamoja na blog hii , newe amesema kwasasa mikoani kuna studio kubwa na zenye vifaa bora zaidi kiasi cha kuzalisha muziki kwa ubora zaidi kuliko hata zilizopo Dar es salaam.

Akiiongelea studio yake ya zero to hero records , mmliki huo alisema kuwa ,wao wananaamini katika ubora kiasi kwamba kwa muda mfupi wamefanikiwa kuzalisha muziki mzuri kiasi cha kutoa ushindani wa hali ya juu kwa studio kongwe na kubwa za audio hapa nchini.

No comments:

Post a Comment