Ads

test

Thursday, December 29, 2016

Mambo 3 ambayo Nandy hawezi kuyasahau kwa mwaka 2016

Katika kuelekea kuumaliza mwaka huu wa 2016 kila mmoja anakuwa na kumbukumbu ya mambo muhimu ambayo yamemtokea ndani ya mwaka hadi kufikia kuumaliza, haijalishi kama ni mazuri au mabaya, yote yanaweza kukaa kwenye kumbukumbu.
Mwanadada Nandy amepiga story na hot n hot site  na kutusanua ni mambo gani ambayo kwa upande wake hawezi kuyasahau kwa mwaka huu wa 2016.
Ni dhahiri kabisa kuwa mwaka huu umekuwa ni wa mafanikio zaidi kwa mwanadada Nandy kutokana na mengi ambayo amekuwa akifanya kwa mwaka huu yamekuwa mswano. Ikiwa ni pamoja na kuwa mmoja kati ya washindi wa shindano la Tecno own The Stage ambalo fainali zake zilifanyika huko nchini Nigeria.
“Cha kwanza ambacho siwezi kukisahau ni jinsi nilivyoshinda kwenda Nigeria kwenye audition za Tecno Own The Stage, na nilivyoshinda kama mshindi wa pili na nilivyopata zile hela, tuzo na simu, hicho ni cha kwanza ambacho sitaweza kukisahau.”
Hicho ni kitu kimoja ambacho Nandy hawezi kukisahau kwa mwaka huu wa 2016, unataka kuvijua vingine viwili? Play hii video hapa chini kumsikiliza mwenyewe akizungumza juu ya mambo hayo.

No comments:

Post a Comment