Ads

test

Tuesday, December 20, 2016

UPEPO MTAMU WA DARASA KWA MWAKA 2016

Kati ya marapa wakali na ambao tunaweza kusema kwa mwaka 2016  wanaumaliza wakiwa na upepo mkubwa sana wa mashabiki na walijozolea mashabiki lukuki kwa mwaka 2016 , Darasa ni mmoja wapo, ambapo aliweza kudhihirisha ukali wake  na ukubwa wake sio wa kubahatisha  bali ni ukubwa ambao ameudhamiria kuutendea haki Nakutendea haki mashabiki zake.Mshikaji alipoachia ngoma ya KAMA UTANIPENDA , aliyofanya kwa Abba process, producer ambaye  kwa kiasi kikubwa ngoma hiyo iliweza kumpaisha zaidi, wengi walihisi darasa asingewewa kutoa ngoma kubwa zaidi ya hiyo au ambayo ingekaribia hiyo, na badala yake akaweza kuwdhibitishia mashabiki kuwa hakuwa anabip na badala yake alijipanga kikamilifu baada ya kuachia jiwe lingine kwa muda mfupi tu , ngoma iliyojulikana kwa jina la too much.
Ngoma ya too much ilipata mapokeo makubwa sana katika mitandao ya kijamii kiasi cha kuvunja record ya ngoma yake aliyoitoa  muda mfupi kabla ya hiyo, ngoma ya KAMA utanipenda .
Kabla ya kuuaga mwaka 2016, joto la ngoma ya too much likiwa halijapoa , mshikaji akaweza kuachia jiwe lingine linalokwenda kwa jina la muziki ngoma ambayo amemshirikisha ben paul, na ikiwa imefanywa na maproducer watatu ambao ni VS, Abba process pamoja na Mr. t touch.
Mapokeo ya ngoma ya muziki yamekuwa ni makubwa zaidi  ya ngoma zake mbili zilizotangulia kiasi cha mashabiki pamoja na watu maarufu wakiwemo  mdj, radio presenters pamoja na  waigizaji, wakiamua kuibatiza jina la wimbo wa taifa .
Darasa anaufunga mwaka 2016 akiwa ni msanii ambaye  ngoma zake zimeeleweka kwa kiasi kikubwa sana kwa mashabiki wake.

 

No comments:

Post a Comment