Ads

test

Monday, December 19, 2016

P the Mc, Mmoja wa marapa waliotoa hit kali 2016

P the mc , ni kati ya marapa wakali wanaotoka chini  ya mwavuli wa tamaduni muziki nchini Tanzania , na ambao ni wakubwa katika   sanaa ya muziki  wa  Tanzania …jamaa ni kati ya wasanii ambao waliweza kuachia ngoma kubwa na kali sana ambayo ilitoka rasmi mwezi wa pili  mwaka huu wa  2016 , ngoma ambayo amemshirikisha   Jux katika kiitikio lakini ikiwa imefanyika chini ya 4.12. (four point twelve )Dully sykes, Ngoma ya Namimi.…ukiwa sio mfuatiliaji sana wa kazi za huyu jamaa   unaweza ukamchukulia kawaida au kumuweka katika level ambazo ni ndogo sana , kulinganisha na anachokifanya , lakini kwa wale wote wanaojua kazi anayoifanya na wanaofuatilia kazi zake ni wazi watakubaliana nami  kwamba jamaa ni mkubwa sana katika sanaa ya muziki especially ya Tanzania na nchi za jirani….
Mwaka 2016 baada ya kuachia ngoma yake ya  “Na mimi” aliyoshirikiana na Jux, aliweza kudhihirishia uma wa watanzania na mashabiki zake kuwa  sio tu ni mkali katika michano kama ambavyo wengi wamemzoea katika upande huo lakini pia   katika nyimbo   anaweza  kufanya kitu kikubwa zaidi  kwa upande wa kuimba au nyimbo za biashara kama ambavyo wengi hivi sasa wamekuwa wakiziita hivyo.
Ngoma yake ya Na mimi, kwa mwaka 2016, iliweza kubadili upepo kiasi cha kujizolea mashabiki lukuki wa upande wa pili ambao si wale waliozoea ngoma ngumu, hivyo kuingia katika mzunguko mkubwa sana wa ngoma zilizoombwa sana katika kipindi chote cha mwaka 2016, na pia kuingia katika list ya ngoma kumi au ishirini bora za vituo mbalimbali vya radio nchini tanzania .
ngoma hiyo pia imeweza kumuwezesha p the mc , kuwa na project nyingi  za mikoani zikiwemo show pamoja na uuzaji wa bidhaa nyingi sana kama kofia, masweta, jumpers, singlend, bodytight pia ambazo zina logo ya Na mimi......


No comments:

Post a Comment