Ads

test

Monday, January 16, 2017

BELLE 9-: SIFIKIRII KUWA NA LEBO

Imekuwa kama fashion hivi kwa wasanii wa Bongo kila mmoja kutaka kumiliki lebo ya muziki na kusimamia wasanii kama ilivyo kwa wachache baadhi ambao wamekwisha fanikiwa katika suala hilo.
Sasa kama uliwaza kuhusu jambo hilo kwa mtu mzima Belle 9 futa kabisa mawazo yako, amefunguka kupitia kipaza cha Hothotsite  kuwa hafikirii kabisa kumiliki lebo na kusimamia wasanii bali anachokiwaza yeye ni kutoa sapoti endapo utahitajika msaada wake.
“Sifikirii kwamba siku moja nimiliki wasanii kibao ambao mimi nitakuwa nawa own, mimi nafikiria kusapot. Kitu ambacho nafikiria ni kuwa na studio ambayo watu wanaweza kupata platform ya kurekodi kwa urahisi kwasababu studio sasa hivi imekuwa kitu cha kawaida, watu wana studio lakini studio ambayo naiongelea mimi ni studio ambayo kila mtu ataweza kuja kurekodi.” ALisema Belle 9.

No comments:

Post a Comment