Ads

test

Monday, January 16, 2017

HARMONIZE AMEAMUA KUFUNGUKA KWANINI MAMA YAKE ANAUPENDA WIMBO WA ‘MATATIZO’

Harmonize ameamua kufunguka kwa mashabiki zake kuwa katika ngoma zote ambazo amewahi kuzifanya, ngoma ya ‘Matatizo’ ndio ngoma ambayo Mama wa Harmonize anaikubali.
Kama kawaida blog hii ilimvutia waya na  ukamnyaka Harmonize na kufunguka kwanini Mama yake anapenda ngoma ya ‘Matatizo’, wakati akiwa ameunyaka waya huo Harmonize alisema kwamba ‘Matatizo’ ndiyo wimbo ambao Mama yake anaupenda kutoka moyoni na ni wimbo ambao kabla haujatoka yeye ndio alikuwa wakwanza kuisikiliza.
“Tangu nianze Muziki, Matatizo ndio wimbo ambao mama yangu anaupenda hadi kesho, naweza nikasema ndio wimbo ambao anauelewa kuliko nyimbo zangu zote kabisa, yaani the way anavyoniambia yaani huu ndio wimbo ambao anaupenda toka moyoni, kwanza matatizo mama yangu alianza kuusikia hata kabla hujatoka kwahiyo alivyousikia ikamjia emotion flani hivi, yaani kuna wakati akawa anaimagine kama ikitokea itakuwaje lakini hakuniambia, ilivyotoka video ndio ikazidi kumgusa kabisa kwasababu nilichokiimba na nilichokifanya kwenye video ndio kile kile…..mwisho wa siku akazoea akaona ni sanaana pia akaendelea kuupenda sana huo wimbo kuliko nyimbo zangu zote” Alisema Harmonize.

No comments:

Post a Comment