Mwanamuziki wa Hip Hop bongo Golden Jacob, maarufu kwa jina la Godzilla
ambaye mwezi december mwaka jana alisherehekea siku yake ya kuzaliwa .
GodZilla amefunguka na kusema kuwa mwaka 2017 yeye ni kazi tu kwani atakuwa akiachia kazi baada ya kazi mpaka mwaka utakapokwisha.

Godzillah amedai kuwa tayari amejipanga kwa mwaka 2017 na ana kazi za
kutosha huku akiwa amejipanga kuongeza vitu vipya zaidi katika muziki
wake ambavyo vitaleta tija na hamasa katika muziki wa hip hop.
“Kwanza nashukuru Mungu kuongeza mwaka mwingine tena lakini mwaka 2017 kwangu mimi ni muziki baada ya muziki, na kuongeza vitu vipya zaidi, cha msingi tuombe uhai” alisema Godzilla ndani ya EATV
Mbali na hilo Godzillah alisisitiza kuwa kuanzia sasa muda wowote ule ataachia kazi yake ya kwanza ambayo ndiyo itakwenda kufungua mwaka 2017 katika muziki wake.

No comments:
Post a Comment